Loading...

Rais Buhari ashinda muhula wa pili kwa kura milioni 15

Wafuasi wa Buhari wakishangilia huko Kano

Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari amechaguliwa kwa muhula mwingine wa miaka minne baada ya masaa kadhaa ya kuhesabiwa kwa kura.

Ameshinda kwa kura millioni 15 akiwa zaid kwa kura millioni 4 zaid ya mpinzani wake Atiku aboubakar .

Upinzani wamekataa matokeo hayo.

Buhari mwenye umri wa miaka 76 amemshida mpinzani wake mkuu na aliyekua makamu wa rais bwana Atiku Aboubakar.

Chama cha Buhari kimeshinda majimbo 19 kati ya 36 , wakati chama cha upinzani cha PDP wakishinda majimbo 17.

Asilimia 35 tuu ya wapiga kura walijitokeza , baadhi wafuasi wa Buhari tayari wameingia mtaani kushangilia.

Buhari aliahidi kushugulikia matatizo ya wanageria kama watamchagua tena

''kama kijana wa Nigeria naamini kuwa huu ni mwanzo mpya kwa nchi yetu, ndo mana tumeamua kumrudisha kwa muhula mwingine'' anasema mfuasi wa Buhari

''nafurahi sana , ni kitu ambacho tuliona kinatokea kuhusu Rais, na ukizungumzia suala la kupambana na rushwa kumesaidia sana, tunajivunia.

Buhari alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 akiwa ni kiongozi wa kwanza wa upinzani kukalia kiti cha urais,

Wakosoaji wake wanasema kuwa amekua akijitetea kusimamia vita ya rushwa na suala la Boko Haram, lakini kwa upande wa uchumi bado kumedorora.

Tume ya uchaguzi imesema kuwa itaangalia malalamiko yote kabla ya kutangaza Rasmi matokeo ya uchaguzi.
Rais Buhari ashinda muhula wa pili kwa kura milioni 15 Rais Buhari ashinda muhula wa pili kwa kura milioni 15 Reviewed by Zero Degree on 2/27/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.