Loading...

Nape Nnauye ajiuzulu


KATIBU wa Bunge, Ndugu Stephen Kagaigai amethibitisha kupokea barua ya mbunge wa Mtama Mh. Nape Nnauye kujiuzulu nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii ili aweze kujikita zaidi katika kuwatumikia wananchi wa Jimbo lake la Mtama.

Kagaigai amesema jana Jumatatu Februari 4, 2019, Nape aliandika barua kwenda kwa Spika wa Bungela Tanzania, Job Ndugai ya kujiuzulu nafasi hiyo na tayari spika amempatia nakala ya barua hiyo.

”Ni kweli nimeiona barua aliyomwamndikia Spika na mimi nimepata nakala yangu kwahiyo ni kweli amejiuzulu labda awe na mawazo mengine”, amesema.

Machi mwaka 2017, Nape aling’olewa kwenye nafasi ya Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambayo sasa ipo chini ya Waziri Harrison Mwakyembe.
Nape Nnauye ajiuzulu Nape Nnauye ajiuzulu Reviewed by Zero Degree on 2/05/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.