Loading...

Sumaye augua ghafla, akimbizwa hospitali


WAZIRI Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ameumwa ghafla akiwa Mkoani Tanga kwenye shughuli za Chama chake cha CHADEMA ambapo yeye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.

Taarifa iliyotolewa na Tumaini Makene imesema amekimbizwa Hospitali ya Bombo na kupatiwa matibabu na inaelezwa kuwa hali yake inaendelea vizuri.

“Mipango ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi inafanyika” Amesema Mkuu wa Idara ya Mawasiliano CHADEMA Tumaini Makene.
Sumaye augua ghafla, akimbizwa hospitali Sumaye augua ghafla, akimbizwa hospitali Reviewed by Zero Degree on 2/08/2019 04:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.