Dudu Baya aachiwa kwa dhamana
Dudu Baya alikamatwa juzi Jumatano na polisi na kufunguliwa jalada la kesi lenye namba OB/RB/2029/2019 la matumizi mabaya ya mitandao.
Hatua hiyo ilikuja baada ya Waziri wa Habari na Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kuagiza Jeshi la Polisi na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kumchukulia hatua mwanamuziki huyo kwa makosa ya kumdhihaki, aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji, Ruge Mutahaba kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Mussa Taibu amesema walimwachia msanii huyo jana Alhamisi, Februari 28 saa 9:00 mchana baada ya kumaliza kumuhoji.
Dudu Baya aachiwa kwa dhamana
Reviewed by Zero Degree
on
3/01/2019 10:50:00 AM
Rating: