Mgeja amfuata Lowassa CCM
Mgeja amedai wakati akiwa katika mapumziko ya kisiasa alijitathimini na kuona sababu zilizomfanya ahamie Chadema wakati wa uchaguzi mwaka 2015 sasa hazipo.
“Nimeamua kurudi nyumbani, sijafuata mkumbo wala kushawishiwa na mtu bali utendakazi wa Serikali yangu ya awamu ya tano umenifanya nirudi. Leo tarehe sita kwa utashi wangu naamua kurudi CCM na sitawaunga mkono tena Chadema,” amesema.

Amesema sababu nyingine inayomfanya atoke Chadema ni kwa sababu chama hicho kimejaa ubinafsi na kisichosikiliza ushauri wa watu wengine.
“Nikiwa Chadema nimewashauri sana waachane na siasa za kiwanaharakati lakini hawakunisikiliza. Sasa ninaomba niwaambie kwa sababu hawakusikiliza ushauri wangu wanakwenda kuwa na anguko kubwa la kisiasa uchaguzi wa 2020,” amesema.
Mgeja aliondoka CCM na kutimukia Chadema mwaka 2015 baada ya Lowassa kujiunga na chama hicho Julai 28, 2015 na kupewa fursa ya kugombea urais.
Mgeja amfuata Lowassa CCM
Reviewed by Zero Degree
on
3/06/2019 07:50:00 AM
Rating: