Loading...

Aussems azungumzia majeraha ya John Bocco, Kagere


Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kati ya Kagera Sugar na Simba mjini Bukoba, kocha wa klabu hiyo, Patrick Aussems amesema kuwa atampumzisha mshambuliaji wake tegemeo, Meddie Kagere katika mchezo huo kutokana na kuumia.

Aussems amesema kuwa kwa sasa mshambuliaji anayemtegemea ni Meddie Kagere ambaye amepata majeraha madogo hivyo atampumzisha ili arejee akiwa bora zaidi.

"John Bocco atakuwa nje kwa wiki nne zaidi na kuhusu Kagere ndiye mshambuliaji wangu pekee kwa sasa, ana majeraha madogo kwahiyo nimempa mapumziko. Ninafarijika kumuona Da Silva anarejea, ameanza mazoezi mepesi na ninafikiri atakuwa mshindani mkubwa dhidi ya Kagera", amesema Aussems.

Simba itavaana na Kagera Sugar Septemba 26 katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba, ambapo katika rekodi za misimu miwili iliyopita, mabingwa hao mara mbili mfululizo wamekutana mara nne na Kagera Sugar na kuambulia ushindi katika mechi moja pekee huku wakifungwa mechi tatu.

Katika msimu wa ligi kuu 2017/18, Simba ilishinda mechi moja na Kagera Sugar ilishinda mechi moja, mechi ambayo Simba ilipoteza mbele ya mgeni rasmi, Rais Dkt. John Magufuli ambaye aliwakabidhi kombe. Msimu uliofuata wa 2018/19, Simba haikufanikiwa kushinda mechi yoyote dhidi ya Kagera Sugar, ikifungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Taifa na kwenye mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Kaitaba, Simba ilifungwa mabao 2-1.
Aussems azungumzia majeraha ya John Bocco, Kagere Aussems azungumzia majeraha ya John Bocco, Kagere Reviewed by Zero Degree on 9/18/2019 08:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.