Loading...

JPM aagiza Askari, Beatrice Mlanzi kupandishwa cheo kwa kuonesha utimilifu kazini

Rais Magufuli alipokuwa akitoa maagizo ya kupandishwa cheo kwa Askari WP 4160 Beatrice Kayuni Mlanzi.


Rais Magufuli ameagiza WP 4160 Beatrice Kayuni Mlanzi, kupandishwa cheo kutoka Koplo na kuwa Sajenti baada ya kuonesha utimilifu katika kazi.

Agizo hilo amelitoa jana Septemba 10, 2019, baada ya kupita katika kituo cha Polisi Selander Bridge.

Rais Magufuli alipita kituoni hapo akiwa njiani kurejea Ikulu, akitokea Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokwenda kumjulia hali Baba Askofu Mkuu Ruwa'ichi.

Rais alimjulia hali Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadeus Ruwa’ichi ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi hiyo ya MOI mara baada ya kufanyiwa upasuaji wa Kichwa.
JPM aagiza Askari, Beatrice Mlanzi kupandishwa cheo kwa kuonesha utimilifu kazini JPM aagiza Askari, Beatrice Mlanzi kupandishwa cheo kwa kuonesha utimilifu kazini Reviewed by Zero Degree on 9/11/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.