JPM azindua rada 2 za kuongozea ndege
Akizungumza katika uzinduzi huo, Jumatatu, Rais Magufuli amesema mradi huo wa rada ni maendeleo makubwa kwa sekta ya anga ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli maendeleo hayo ya sekta ya anga ni muhimu pia kwa shirika la ndege la taifa ATCL ikizingatiwa kuwa hapo awali lilikuwa linashikilia asilimia 3 tu ya soko lakini sasa linashikilia asilimia 75 ya soko la ndani.
“Uwepo wa mradi huu wa rada utavutia mashirika mengi zaidi kuleta ndege zao nchini na hivyo watalii wataongezea, ndege zinazokatiza anga nchini Tanzania pia zitaongezeka hivyo tutaongeza mapato kutokana na tozo za kuongozea ndege,” amesema.

Mradi huo wa rada ni wa thamani ya bilioni 67.3/- fedha ambazo zimetolewa na serikali kutokana na kodi wanazolipa wananchi.
JPM azindua rada 2 za kuongozea ndege
Reviewed by Zero Degree
on
9/16/2019 11:05:00 AM
Rating: