Loading...

Kocha Arsenal: Watford walikuwa bora zaidi yetu


Kocha wa Arsenal Unai Emery amedai Watford ilikuwa bora zaidi yao katika mchezo walitoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Arsenal jana iliduwazwa baada ya Watford kupata penalti dakika ya 81 iliyofungwa na Roberto Pereyra. Bao jingine lilifungwa na Tom Cleverley.

Nahodha wa Gabon, Pierre Emerick-Aubameyang, aliyekuwa nyota wa mchezo, alifunga mabao mawili ya Arsenal.

“Kwa utimamu wa mwili walikuwa bora zaidi yetu. Tuna vijana wadogo wanaendelea kujifunza na wanapata uzoefu kama huu wa leo (jana),” alisemas Emery.

Kocha huyo wa zamani wa Paris Saint Germain (PSG), alisema wamefanya makosa na wanatafuta namna ya kurekebisha.

Kocha wa Watford, Sanchez Flores alidai amevutiwa na kiwango bora cha wachezaji wake waliocheza kwa kujiamini.
Kocha Arsenal: Watford walikuwa bora zaidi yetu Kocha Arsenal: Watford walikuwa bora zaidi yetu Reviewed by Zero Degree on 9/16/2019 07:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.