Loading...

Algeria kufanya uchaguzi wa rais mwezi Disemba


Algeria imetangaza tarehe mpya ya uchaguzi wa urais nchini humo miezi mitano baada ya kuachia ngazi kwa Rais Abdelaziz Bouteflika.

Katika tangazo alilolitoa kupitia televisheni ya taifa rais wa mpito wa nchi hiyo Abdelkadir Bensalah amesema uchaguzi utafanyika tarehe kumi na mbili Disemba.

Bouteflika alikuwa mamlakani kwa zaidi ya miaka ishirini ila akaamua kujiuzulu mwezi Aprili baada ya wiki kadhaa za maandamano yaliyokuwa yakipinga utawala wake.

Awali rais mpya alikuwa amepangiwa kuchaguliwa mwezi Julai ila uchaguzi huo uliahirishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kutokuwepo na wagombea.

Vyama vya upinzani pamoja na waandamanaji walipinga hatua hiyo wakisema kwamba jeshi lilikuwa linataka kutumia hali hiyo kwa manufaa yake.
Algeria kufanya uchaguzi wa rais mwezi Disemba Algeria kufanya uchaguzi wa rais mwezi Disemba Reviewed by Zero Degree on 9/16/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.