Loading...

January, Nape waibua mjadala mitandaoni


Wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Nape Nnauye (Mtama) na January Makamba (Bumbuli) wameibua mjadala kutokana na ujumbe walioandika katika akaunti zao za Twitter.

Nape na Makamba ambao walikuwa mawaziri, wamewekwa kando kwa nyakati tofauti na kwa siku za hivi karibuni wamekuwa na mvuto kwa macho ya Watanzania wengi.

Mvuto huo umeongezeka zaidi baada ya siku za hivi karibuni kumuomba radhi Rais John Magufuli kutokana na kuvuja kwa mazungumzo yao ya simu waliyokuwa wakimteta mkuu huyo wa nchi.

Jana, Septemba 15, 2019, Nape aliyekuwa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter: “Nikumbushe wema wako nisije laumu, nikumbushe ukuu wako wakati wa magumu, nikumbushe shuhuda zako ili nikusifu…niimbie sifa katikati ya machozi.”

Wakati Nape akiandika hayo, Makamba aliyekuwa waziri wa muungano na mazingira ameandika: People who are real never broadcast that they are real.” (Watu ambao ni wa kweli kamwe hawatangazi kuwa wao ni wa kweli).

akichangia ujumbe huo, Isack Mackphason @mackphason amesema, “lakini kupiga magoti wanaweza.”
January, Nape waibua mjadala mitandaoni January, Nape waibua mjadala mitandaoni Reviewed by Zero Degree on 9/16/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.