Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Septemba 16, 2019


Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester United, Nemanja Matic, mwenye umri wa miaka 31, yuko kwenye rada ya Juventus huku kukiwadia kinachowezekana kuwa ni mageuzi ya Januari. (Mirror)

Real Madrid na Barcelona zinatarajiwa kushindana pakubwa kuwania kumvutia meneja Jurgen Klopp na mlinzi Virgil van Dijk, mwenye umri wa miaka 28, kutoka Liverpool. (AS)

Manchester United imejitolea kumfanya kipa David de Gea, mwenye umri wa miaka 28, kuwa mcheza soka anayelipwa pakubwa katika ligi kuu ya England katika kumshawishi kusaini mkataba mpya wa muda mrefu. (Times)

Christian Eriksen anapuuzia mkataba mpya anaopendekezewa na Tottenham wakati wakala wa mchezaji huyo wa kiungo cha kati mwenye miaka 27akishughulikia uhamisho kwenda Real Madrid msimu ujao wa joto. (Marca)

Arsenal inakaribia kufanikiwa kumsajili kijana wa Sunderland Logan Pye baada ya mchezaji huyo wa miaka 15 kuhusishwa ma uhamisho kwenda katika ligi kuu ya England wakati wa msimu wa joto.

Mchezaji wa kiungo cha mbele Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 28, na kipa Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 27, wanamtaka N'Golo Kante - Real Madrid, baada ya mchezaji huyo wa kiungo cha kati wa Chelsea mwenye miaka 28, kuhusishwa na uhamisho kwenda Uhispania. (Sun)

Huenda Real Madrid ikamkabidhi mchezaji wa kiungo cha kati Toni Kroos, kwa Manchester United ili kwa upande wake ijipatie mchezaji wa kiungo cha kati mwenye umri wa miaka 26 Paul Pogba. (FourFourTwo)

Baada ya kuwasajili wachezaji 12 katika uhamisho wa msimu wa joto, mipango imeidhinishwa kwa Aston Villa kushughulika kwa mara nyingine katika dirisha la Januari. (Birmingham Mail)

Vedat Muriqi


Manchester United ilituma mawakala kumchunguza mshambuliaji wa Kosovo, Vedat Muriqi, mwenye umri wa miaka 25, wakati alipofunga dhidi ya timu ya England huko Wembley Jumanne usiku. (Express)

Meneja wa Arsenal, Unai Emery amefichua kwamba alikuwa na Javi Gracia wakati Watford ilipomfuta kazi. (Metro)

Bingwa wa Manchester United Gary Neville amesema anaweza 'kukimbia maili moja' iwapo atapewa kazi ya U meneja Old Trafford. (Manchester Evening News)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Septemba 16, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumatatu Septemba 16, 2019 Reviewed by Zero Degree on 9/16/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.