Manula: Sina wasi wasi na Kaseja
Manula ametemwa katika kikosi hicho kinachojiandaa kucheza na Sudan keshokutwa katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika kwa wachezaji wa Ligi ya Ndani (Chan), utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Bingwa, Manula alisema anatambua ubora wake wa kukaa langoni, lakini wakati mwingine kuna kupokezana majukumu ndani ya kikosi chao cha Simba na Taifa Stars.
Alisema siku zote anamkubali Kaseja kutokana na umahiri wake wa kudaka na uzoefu alionao, hivyo ana matumaini makubwa ya kuipa mafanikio Stars katika mchezo huo.
“Unapozungumzia timu ya taifa maana yake umegusa Watanzania wanaohitaji matokeo mazuri, nawaombea baraka kwa wote walioitwa Stars wakafanye kazi kubwa.
“Sina wasi wasi na Kaseja, ameaanza muda mrefu kudaka kabla yangu na mafanikio yake yameonekana namtakia baraka tele akafanye vizuri kwa niaba ya Watanzania,” alisema Manula.
Manula alisema kwa sasa akili yake imezama zaidi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Septemba 26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Kipa huyo alisema anahitaji kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya na vizuri na hatimaye kutetea taji lao. Alisema watataendelea kupambana ili mwakani waweze kushiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mwaka huu, kutolewa hatua ya awali na timu ya UD Songo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Bingwa, Manula alisema anatambua ubora wake wa kukaa langoni, lakini wakati mwingine kuna kupokezana majukumu ndani ya kikosi chao cha Simba na Taifa Stars.
Alisema siku zote anamkubali Kaseja kutokana na umahiri wake wa kudaka na uzoefu alionao, hivyo ana matumaini makubwa ya kuipa mafanikio Stars katika mchezo huo.
“Unapozungumzia timu ya taifa maana yake umegusa Watanzania wanaohitaji matokeo mazuri, nawaombea baraka kwa wote walioitwa Stars wakafanye kazi kubwa.
Juma Kaseja |
Manula alisema kwa sasa akili yake imezama zaidi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa Septemba 26, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Kipa huyo alisema anahitaji kufanya kazi ya ziada kuhakikisha anaisadia timu yake kufanya na vizuri na hatimaye kutetea taji lao. Alisema watataendelea kupambana ili mwakani waweze kushiriki michuano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya mwaka huu, kutolewa hatua ya awali na timu ya UD Songo.
Manula: Sina wasi wasi na Kaseja
Reviewed by Zero Degree
on
9/20/2019 10:35:00 AM
Rating: