Loading...

Pirlo ataja jina la mrithi wake



Aliyekuwa kiungo wa klabu ya AC Milan na Juventus Andrea Pirlo amiepa nafasi Juventus kutwaa ubingwa wa Serie A kwa mara nyingine tena na kumtaja mchezaji ambaye ana uwezekano mkubwa wa kufuata katika nyayo zake, naye si mwingine ni nyota wa klabu ya Barcelona Frenkie de Jong.

Mkongwe huyo, ambaye ameshastaafu soka kama mchezaji alizungumza na Radio Bianconera kuhusiana na muda wake alipokuwa Turin na wachezaji wengi ambao wamekuwa wakilinganishwa na kiwango chake tangu wakati huo.

“Wakati nilipujiunga na Juventus, nilifanya vile kufungua ukurasa wa mataji. Nilishawishika kabisa kuwa hilo lingewezekana, mbali na hivyo ningeondoka.

“Hata kama inaweza kuonekana kuwa ni vita yenye mlinganyo kati ya Inter na Napoli kufuatia usajili wao mpya. Juventus wanahitaji muda mfupi wa kufanya mabadiliko kidogo kwa kocha na wachezaji pia, hivyo tusubiri baada ya muda mfupi tuone, lakini Juve wanabakia kuwa chaguo langu.”

Wachezaji wengi wametajwa kuwa “Pirlo mpya,” lakini kwa upande wake yeye alipoulizwa ni mchezaji gani anahisi ndiye?

Frenkie De Jong, 22



“Mchezaji pekee ambaye kiasi flani naweza kumtaja ni De Jong. Miralem Pjanic anazo sifa kadhaa kwenye staili ya uchezaji wake, lakini tunatofautiana na kila mtu ana staili yake.”

Barcelona ililipa kiasi cha kaibu pauni milioni 75 kwenye msimu huu wa majira ya joto kumsajili nyota huyo kutoka Uholanzi Frenkie De Jong, 22 kutoka Ajax. Hivi karibuni alikuwa mchezaji pekee aliyejitokeza kwenda mbele ya mashabiki wa klabu hiyo kuomba msamaha kufuatia kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Granada kwenye La Liga na wa kwanza kufanya mahojiano na vyombo vya habari.
Pirlo ataja jina la mrithi wake Pirlo ataja jina la mrithi wake Reviewed by Zero Degree on 9/27/2019 06:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.