Loading...

Argentina: Kifo cha Diego Maradona chaibua uchunguzi



Maofisa nchini Argentina wameanza uchunguzi wa kifo cha Diego Maradona kama kilichangiwa na uzembe wa kitabibu, imeelezwa.

“Kuna uwezekano wa kutokuwa kifo cha kawaida,” mmoja wa wanafamalia y AFP.

Awali, Wakili wa Maradona, Matias Morla aliomba kufanyike uchunguzi juu ya madai ya kuchelewa kwa gari la wagonjwa kuchukua zaidi ya nusu saa hadi kufika nyumbani kwa nyota huyo wa soka licha ya kupigiwa simu siku aliyokufa.

Taarifa za awali zilieleza kuwa Maradona alikufa akiwa usingizini Jumatano mchana kutokana na tatizo la moyo kushindwa kufanya kazi vizuri (heart failure).

Maofisa usalama mjini Buenos Aires walifungua jalada kuhusu jina la ‘Maradona, Diego. Kuhusiana na sababu za kifo.’

“Faili hilo limepewa jina hilo kutokana na kuwa mtu aliyefia nyumbani na hakuna mtu yeyote aliyesaini hati yake ya kifo. Ingawa haina maana kuwa kunaweza kuwa na uzembe,” chanzo ndani ya ofisi ya wachunguzi kilisema.

Mchezaji huyo wa zamani wa Argentina alifariki Jumatano akiwa na miaka 60, akiwa pia na matatibabu yaliyokuwa yakiendelea nyumbani kwake mjini Tigre, Kusini mwa jiji la Buenos Aires, alipokuwa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kichwa mapema mwezi huu.

“Tunatakiwa kuangalia kama walifanya (wauguzi) kile ambacho walitakiwa kukifanya kwa muda sahihi, au walipuuza,” mmoja wa wanafamilia aliiambia AFP.

“Muuguzi aliandaa maelezo yake, wakati maofisa wa usalama walipofika siku ya kifo cha Diego, kisha nesi aliongeza katika taarifa hiyo na kisha kuzungumza na tv na kusema walichokiandika hakikuwa sawa, hivyo kuna kujichanganya katika taarifa yake,” the close relative said.

Maofisa hao wanasubiri baadhi ya vipimo vilivyofanyika kutoka katika mwili wa Maradona.

Maofisa watatu wanaoshughulikia suala hilo waliomba rekodi ya mgonjwa huyo (Diego), pamoja na picha za video za kamera zilizokuwa nyumba za jirani.

Nesi mwingine aliyekuwa na kazi ya kumwangalia Maradona anaonekana kuwa mtu wa mwisho kumwona nyota huyo akiwa mzima, Jumatano asubuhi, taarifa ya maofisa wao ilisema jana.

“Kutoka katika maneno yake, inaonekana kuwa alikuwa mtu wa mwisho kumwona (Maradona) akiwa hai, ilikuwa saa 12:30 asubuhi, wakati muda wake wa kumwangalia nyota huyo ukiwa umekwisha,” iliendelea kusema taarifa ya jana ya maofisa wanaochunguza kifo hicho.
Argentina: Kifo cha Diego Maradona chaibua uchunguzi Argentina: Kifo cha Diego Maradona chaibua uchunguzi Reviewed by Zero Degree on 11/30/2020 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.