Bei za vyakula zapanda kwa kiwango cha juu
Shirika la chakula na kilimo ulimwenguni, FAO limesema bei ya bidhaa za vyakula imepanda kwa mwezi wa sita mfululizo, ikigonga kiwango cha juu kabisa tangu Desemba 2014.
Ripoti ya shirika hilo imesema janga la virusi vya corona limekuwa kichochezi kikubwa cha ukosefu wa usawa wa chakula ulimwenguni pamoja na mabadiliko ya tabianchi. Bei ya chakula imeongezeka mwezi Novemba kwa kiwango ambacho hakikuwahi kushuhudiwa kwa takriban miaka sita.
Faharasa inayochapishwa kila mwezi na FAO hapo jana imeonyesha bei za bidhaa kadhaa za chakula kuongezeka mno mwezi Novemba. Bidhaa ambayo imepanda bei zaidi ni mafuta ya kupikia. Kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya mawese, bei ya mafuta ya kupikia imeongezeka kwa asilimia 14.5. Bei za vyakula vya nafaka, sukari, nyama na maziwa pia zimeongezeka.
Bei za vyakula zapanda kwa kiwango cha juu
Reviewed by Zero Degree
on
12/04/2020 11:35:00 AM
Rating: