Loading...

Maji safi kupatikana kwa 100% ifikapo mwaka 2030

Wadau wa maji kutoka ndani na nje ya nchi walikutana leo jijini Dar es salaam kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu upatikanaji wa maji safi na salama sambamba na utatuzi wa changamoto za sekta ya maji mijini na vijijini.


Serikali imesema ifikapo 2030 upatikanaji wa maji safi na salama utakuwa wa asilimia mia moja.

Pia mpaka sasa miradi ya maji takribani 1,423 imekamilika
licha ya kuwa bado kuna baadhi ya maeneo yana changamoto za
upatikanaji wa maji hasa maeneo ya vijijini.

Hayo yameelezwa leo Desemba 3, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Injinia Antony Sanga wakati alipokutana na wadau wa maji kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo amesema mpaka sasa serikali imefanya kazi ya kuhakikisha maeneo mengi nchini yanakuwa na maji safi na salama ya uhakika.

Wadau wa maji kutoka ndani na nje ya nchi walikutana leo jijini Dar es salaam kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu upatikanaji wa maji safi na salama sambamba na utatuzi wa changamoto za sekta ya maji mijini na vijijini.

Injinia Sanga amesema kuwa miradi mingi imekaqmilika na kwamba
upatikanaji wa maji katika meneo ya vijijini ni kwa asilimia 70 huku
maeneo ya mijini ni kwa asilimia 80 huku lengo ikifika 2030 kuwepo na
upatikanaji wa maji sawa kwa asilimia 100.

“Katika uongozi wa Rais Dk. John Magufuli tumepambana na kuhakikisha maji
kwa asilimia kubwa yanapatikana licha ya kwamba kuna changamoto ndogondogo ambazo tunahakikisha ifikapo 2030 kila kitu kitakuwa sawa,’’ amesema.
Naye Mwenyekiti wa jukwaa la watumiaji wa maji Injinia Mbogo Futakamba alisema hali ya usambazaji wa m,aji nchini unaridhisha licha ya kwamba kuna maeneo bado yanaupotevu wa maji.

Amesema kwa sasa udhibiti wa upotevu wa maji upo kwa asilimia 30 mapaka 35 lakini lengo ushuke mpaka kufikia asilimian 20 mapaka 25.
Maji safi kupatikana kwa 100% ifikapo mwaka 2030 Maji safi kupatikana kwa 100% ifikapo mwaka 2030 Reviewed by Zero Degree on 12/04/2020 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.