Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Disemba 4, 2020
Mlinzi wa Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 27, na mlinzi wa England Fikayo Tomori, 22, wanaweza kuondoka kwenye klabu hizo wakati wa kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari.
Rudiger alicheza mchezo mmoja tu wa kwanza wa Primia Ligi msimu huu, huku Tomori akiwa bado hajacheza hata mechi moja kubwa ya 2020-2021.
Barcelona imeanza mazungumzo na mshambuliaji wa kati Mfaransa, Ousmane Dembele kuhusu mkataba mpya , huku Manchester United nao wakiendelea kumsaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (ESPN)
Tottenham, Everton na Atletico Madrid wanamuangalia kwa karibu kwa lengo la kumnunua mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Napoli Arkadiusz Milik, 26 raia wa Poland. (AS)
West Ham wanamsaini mlinzi wa kikosi cha Denmark cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Frederik Alves Ibsen, 20, kutoka Silkeborg kwa garama ya pauni milioni 1.2 mwezi Januari. (Sky Sports)
Arsenal na Liverpool wanaangalia uwezekano wa kumhamisha kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma, 24.
Manchester United wanapaswa kumfuta kazi meneja wa klabu hiyo Ole Gunnar Solskjaer na nafasi yake ichukuliwe na ama Mauricio Pochettino, Antonio Cone au Diego Simeone, anasema mmiliki wa wa zamani wa Crystal Palace Simon Jordan. (Talksport)
Wayne Rooney ameendelea kusema kuwa bado anapendelea kuwa meneja wa kudumu katika klabu ya Derby County, licha ya mchezaji mwenzake wa zamani katika England John Terry kuhusishwa na kazi yake. (Goal)
Wayne Rooney ameendelea kusema kuwa bado anapendelea kuwa meneja wa kudumu katika klabu ya Derby County, licha ya mchezaji mwenzake wa zamani katika England John Terry kuhusishwa na kazi yake. (Goal)
Arsenal wanatakiwa kumsaini mshambuliaji wa kati wa Crystal Palace raia wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 28, anasema David Seaman, ambaye alishinda mataji matatu ya ligi na vikombe vinne vya FA akiwa na Gunners. (Evening Standard)
Meneja wa Tottenham Jose Mourinho, 57, anaamini kuwa bado ana miaka ''15 hadi 20 " iliyobaki katika kazi yake ya kufundisha, ikimaanisha kuwa anataka kuwa bado ni meneja wa soka akiwa na miaka 70 na zaidi . (iSport)
Wakati huo huo, kiungo wa kati wa Arsenal Muruguay Lucas Torreira, 24, bado ana muda wa mchezo katika siku zijazo katika Gunners licha ya kucheza kwa mkopo katika Atletico Madrid, anasema Gilberto Silva, aliyeshinda taji moja la Primia Ligi na vikombe viwili vya FA Cups akiwa na Gunners. (Sun)
Newcastle United wanataka kumsaini mlinzi wa Manchester United kutoka kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21-Brandon Williams, 20, ambaye bado hajaanza mchezo wa Primia Ligi katika 2020-21. (Star)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Disemba 4, 2020
Reviewed by Zero Degree
on
12/04/2020 08:50:00 AM
Rating: