Loading...

Mama avunja ukimya kuhusu ndoa ya Ali Kiba na mkewe


Mama wa Ali Kiba amevunja ukimya kuhusu uhai wa ndoa ya mtoto wake Ali Kiba na kusema mkewe, Amina Khaleef yupo likizo ya mapenzi kwa sasa.

Ali Kiba ambaye ni msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania na Amina walifunga ndoa Aprili mwaka 2018 na tangu kufunga kwao ndoa kumekuwepo na sintofahamu kwamba wawili hao bado wapo pamoja au la kutokana na kutoonekana mara kwa mara wakiwa pamoja.

Mama Kiba ameyasema hayo leo Ijumaa Februari 5, 2021 alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Leo Tena katika kituo cha redio Clouds.

Kati ya mambo ambayo wasikilizaji walitaka kujua kutoka kwa mama huyo ni kama bado ndoa ya Ali Kiba na Amina na kama wanaishi pamoja au la, kwani kumekuwepo na tetesi kwa muda mrefu kuhusu kuachana kwa wawili hao.

Akijibu swali hilo, mama Kiba amesema mrembo huyo kutoka nchini Kenya ndoa yao bado ipo japokuwa kwa sasa yupo katika likizo ya mapenzi.

Alipoombwa kufafanua kauli hiyo, amesema ”Kusema Amina yupo likizo ya mapenzi naamanisha amemuomba mume wake kwenda kumsalimia mama yake, jambo ambalo amekuwa akilifanya mara kwa mara hata wanapokuja ndugu zake ambao wanaishi nje ya nchi na mimi nina taarifa hiyo kwani aliniaga,” amesema.

Kuhusu kuwepo kwa ugomvi kati yake na mkwe wake huyo, mama Kiba alikanusha na kusema wapo vizuri na kutaka asiyeamini amuulize hata leo mwanamke huyo.
Mama avunja ukimya kuhusu ndoa ya Ali Kiba na mkewe Mama avunja ukimya kuhusu ndoa ya Ali Kiba na mkewe Reviewed by Zero Degree on 2/05/2021 01:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.