Loading...

Madiwani wakerwa vyoo vya kisasa shuleni kutokuwa na maji



MADIWANI wa halmashauri ya wilaya ya Tarime wamesema kuwa ukosefu wa maji kwenye vyoo katika shule za msingi na sekondari ni kero kwa wanafunzi na inahatarisha usalama wa afya,hivyo wameiomba halmashauri kutafuta ufumbuzi wa upatikanaji wa maji shuleni.

Wakizungumza kwenye kikao cha baraza la madiwani, diwani wa kata Nyarero John Mhabasi alisema kuwa baadhi ya shule zina vyoo vilivyojengwa kisasa vinavyotakiwa kutumia maji lakini hakuna maji hali inayosababisha vyoo kuwa vichafu.

"Tatizo la maji shuleni litakwisha lini?vyoo vimejengwa kisasa vinavyohitaji maji lakini maji ya kusafisha choo hakuna na wanafunzi wanapata shida wanahangaika wanapotaka kujisaidia,je kamati husika inamkakati gani kuondoka tatizo la maji shuleni ?alihoji Muhabasi.

Diwani wa viti maalumu Nyamongo Felister Range alisema kuwa changamoto ya maji inazikabili shule nyingi za msingi na sekondari ikiwemo shule ya Sekondari Nyamongo,lakini pia baadhi ya shule wanafunzi wanalazimika kutoka na maji nyumbani kupeleka shuleni.

Diwani wa kata ya Nyansincha Samwel Muhono alisema kuwa ukosefu wa maji shuleni imekuwa kero kwa wanafunzi kwani ulazimika kuyatafuta maji mtoni na kwenye visima kupeleke shule jambo ambalo wakati mwingine wanachelewa shule kwasababu yakwenda kutafuta maji hasa kipindi cha kiangazi ambapo maji ya kuvuna ya mvua kwenye baadhi ya matenki ya shule yanakuwa yamekwisha.

Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya Elimu,Afya na Maji ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mwema Petro Kurate alisema kuwa halmashauri haijatenga bajeti ya kupeleka maji shuleni" tunaweza kuweka bajeti ya maji shuleni alafu maji yasipatikane,idara ya elimu ifatilie kwanza kujua maeneo ambayo maji yatapatikana.

Diwani wa kata ya Nyanungu Tiboche Richard yeye alitaka kufahamu sababu ya kiwanda kilichokuwa kikijengwa cha kuchakata zao la ndizi kwenye kata hiyo lakini kikasimamishwa,nakudai kuwa kiwanda hicho kikijengwa kitakuwa na manufaa kwa wakulima kwa kuuza mazao yao,ajira na halmashauri itapata mapato ya ndani.

Mwenyekiti wa kamati ya ya Uchumi na ujenzi ambaye ni diwani wa kata ya Matongo Godfrey Kegoye alisema kuwa kamati ilikwisha jadili na kutoa maelekezo juu ya kiwanda hicho baada ya kutembelewa lakini anashangaa kwanini ujenzi haujaanza.

Afisa kilimo halmashauri ya wilaya ya Tarime Sylvanus Gwiboha alisema kuwa kiwanda hicho kinamilikiwa na mtu binafsi baada ya kutembelewa kilikutwa na mapungufu na mmiliki alitumiwa barua ya kusimamisha ujenzi hadi atakapotekeleza maelekezo jambo ambalo hadi sasa hajalifanyia utekelezaji.

Pia baadhi ya Madiwani akiwemo Diwani wa kata ya Gwitiryo Nashoni Mchuma waliilalamikia Idara ya Maendeleo ya jamii kuwa maafisa wa idara hiyo wamekuwa wakitoa kauli zisizo rafiki kwa wananchi hususani wa kata yake wanaofika kuomba mikopo jambo linalowafanya baadhi yao kukata tamaa na kuacha kuomba mikopo ya halmashauri.

Chanzo: Nipashe
Madiwani wakerwa vyoo vya kisasa shuleni kutokuwa na maji Madiwani wakerwa vyoo vya kisasa shuleni kutokuwa na maji Reviewed by Zero Degree on 11/03/2021 06:15:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.