Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Novemba, 2021


Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uingereza na Tottenham Harry Kane, 28, ataachana na mipango ya kuondoka katika klabu hiyo baada ya kuwasili kwa Antonio Conte kuifundisha klabu hiyo.

Unai Emery amejiondoa katika kinyang'anyiro cha kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Newcastle , akisema kwamba yuko asilimia 100 katika klabu ya Villareal.

Mkufunzi huyo wa zamani wa Arsenal alithibitisha siku ya Jumanne kwamba alikuwa amewasiliana na maafisa wa klabu hiyo ya ligi ya Premia , ambao walimpatia fursa ya kwanza kuchukua mahala pake Steve Bruce.

Newcastle wanapanga uhamisho wa huru kwa mchezaji wa Inter Milan Marcelo Brozovic huku kiungo mkabaji wa Croatia, 28, akimaliza mkataba wake msimu ujao.

Kiungo wa kimataifa wa Uingereza Fabio Carvalho amekataa ofa 'kubwa' ya kusalia Fulham huku winga huyo mwenye umri wa miaka 19, ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid, sasa mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu huu. (Sun)

Conte anajiandaa kwa usajii wa kwanza wa kiungo wa kati wa AC Milan Franck Kessie, akiwa kocha wa Tottenham. (Metro)

Licha ya Unai Emery kuwa kipenzi, kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez anahimizwa kubeba mikoba ya kocha wa Newcastle na kocha wa muda Graeme Jones, ambaye hapo awali alikuwa msaidizi wa Mhispania huyo akiwa Ubelgiji.

Conte pia anaitaka Tottenham imsajili Mholanzi anayecheza nafasi ya Ulinzi Inter Milan, Stefan de Vrij,29 mwezi Januari. (Football Insider)


Paul Pogba wa Manchester United anapendelea kurejea Juventus badala ya kujiunga na Paris St-Germain au Real Madrid wakati kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 28, atakapokuwa mchezaji huru msimu ujao.(Gazzetta dello Sport)

Erling Braut Haaland ameamua kuondoka Borussia Dortmund na wakala wake anataka mshambuliaji huyo wa Norway, 21, ajiunge na Barcelona.(El Nacional)

Borussia Dortmund, wana imani kwamba wataendelea kumfuatilia Haaland wa Manchester City na Chelsea, licha ya sharti la kitita cha pauni milioni 64 kumnasa mchezaji huyo kuanzia mwaka ujao. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Real Madrid Eden Hazard anaweza kujiunga na Newcastle wakati wa dirisha la usajili mwezi Januari, huku Carlo Ancelotti akijiandaa kumuachia Mbelgiji huyo, 30. (Star)

Tottenham, West Ham na Southampton zinamfukuzia mlinda mlango wa West Brom Sam Johnstone, 28, ambaye mkataba wake utakwisha majira yajayo ya joto. (Sky Sports)

Tottenham wako tayari kuchuana na Juventus kumnasa mshambuliaji wa Fiorentina, Mserbia Dusan Vlahovic,21. (Calciomercato)

Christian Eriksen yuko tayari kujiunga tena na Ajax mnamo Januari kwani kiungo huyo wa kati wa Denmark, 29, hawezi kuichezea klabu yake ya sasa ya Inter Milan akiwa amewekewa kifaa cha moyo cha kudhibiti mapigo ya moyo. (Corriere dello Sport)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Novemba, 2021 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Novemba, 2021 Reviewed by Zero Degree on 11/03/2021 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.