Loading...

Wahamiaji haramu zaidi ya 1000 wakamatwa mkoani Kagera

Mkuu wa Uhamiaji Kagera, Thomas Fussy


IDARA ya Uhamiaji mkoani Kagera imewakamata wahamiaji haramu 1,152 katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka huu, baada ya kubainika kuingia kinyemela katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na namna gani idara hiyo inakabiliana na tatizo la watu wasio raia kuingia hapa nchini bila kufuata utaratibu, mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kagera Thomas Fussy amesema kuwa wahamiaji 1,133 wamerejeshwa nchini mwao na wengine tisa wamefikishwa mahakamani.

Fussy amesema kuwa wamefikia uamuzi wa kurejesha idadi kubwa ya wahamaji hao nchini mwao ili kuepusha kuongeza msongamano katika magereza, kutokana na uwepo waugonjwa wa Uviko 19.

"Wahamiaji waliokamatwa ni kutoka katika nchi za Burundi wahamiaji 912, Uganda 194, Wanyarwanda 35, Wakongo watano, Wasomali watatu, huku Ethiopia, Kenya na Nigeria wakikamatwa wahamiaji mmoja kila nchi" amesema. Fussy amewataka raia wa nchi jirani wanaotaka kuingia hapa nchini kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria, vinginevyo wakikamatwa wameingia kwa njia za panya watachukuliwa hatua kali.
Wahamiaji haramu zaidi ya 1000 wakamatwa mkoani Kagera Wahamiaji haramu zaidi ya 1000 wakamatwa mkoani Kagera Reviewed by Zero Degree on 11/03/2021 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.