Loading...

George Lwandamina 'out' Azam FC



MZAMBIA George Lwandamina amejiuzulu ukocha wa Azam FC siku moja baada ya timu hiyo kulazimishwa sare ya 0-0 na Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Lwandamina aliyewahi pia kufundisha Yanga ya Dar es Salaam, ameiandikia barua Bodi ya Azam FC na kuishukuru kwa nafasi iliyompa klabuni.

Katika barua yake, kocha huyo wa zamani wa Zesco United ya kwao, Zambia amesema amechukua uamuzi huo kwa maslahi ya klabu.

Uongozi wa klabu umeridhia hatua hiyo na moja kwa moja umemteua Mkurugenzi wa ufundi, Mmarekani mwenye asili ya Somalia, Abdihamid Moalin kukaimu nafasi hiyo hadi atakapotangazwa kocha mpya.

Lwandamina alijiunga na Azam  Desemba mwaka jana kuchukua nafasi ya Mromania, Aristica Cioaba.

Ameiongoza Azam FC kwenye mechi rasmi 38; zikiwemo 30 za ligi kuu, nne za Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) na nne za Kombe la Shirikisho Afrika.
George Lwandamina 'out' Azam FC George Lwandamina 'out' Azam FC Reviewed by Zero Degree on 12/14/2021 08:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.