Loading...

Simba yaahidi kufanya makubwa kwenye dirisha dogo



UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kwenye dirisha dogo la usajili watafanya usajili wa maana kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Pablo Franco.

Dirisha dogo la usajili limefunguliwa Desemba 16 na linatarajiwa kufungwa Januari 15,2022 ambapo kwa sasa timu zimeanza harakati za usajili.

Mwenyekiti wa Simba, Murtanza Mangungu alisema kuwa mipango ipo na wanahitaji kufanya jambo zuri kwa ajili ya timu hiyo.

“Tunajua kwamba wengi wanataka kusikia tutafanya nini kwenye wakati huu wa usajili, hatuna presha na jambo lolote,tutafanya usajili wa maana na mzuri.

“Kikubwa ni kuwa na subira unajua mambo mazuri hayahitaji haraka na kwa na kila kitu kinahitaji mikakati imara,” alisema Mangungu.

Chanzo: Championi
Simba yaahidi kufanya makubwa kwenye dirisha dogo Simba yaahidi kufanya makubwa kwenye dirisha dogo Reviewed by Zero Degree on 12/21/2021 11:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.