Loading...

Algeria kutoa pesa kwa wananchi wasiokuwa na ajira



Rais wa Algeria amesema serikali itaanzisha mpango wa kutoa pesa kwa watu wazima ambao hawana ajira, wakati nchi hiyo inakabiliwa na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira.

Rais Abdelmadjid Tebboune amewaambia waandishi wa habari kwamba watu wanaotafuta ajira wenye umri wa miaka kati ya 19 na 40 wataanza kupewa pesa za matumizi kuanzia mwezi machi mwaka 2022.

Watapewa dola za Marekani 73 kwa mwezi pamoja na huduma ya afya hadi watakapopata ajira.

Wakati akitoa tangazo hilo Tebboune amesema kwamba Algeria itakuwa nchi ya kwanza nje ya Ulaya kutekeleza mpango kama huo.

Ameongea kwamba nchi hiyo ina zaidi ya watu 600,000 ambao hawana ajira.
Algeria kutoa pesa kwa wananchi wasiokuwa na ajira Algeria kutoa pesa kwa wananchi wasiokuwa na ajira Reviewed by Zero Degree on 2/16/2022 11:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.