Loading...

Ajali ya boti yauwa zaidi ya watu 90 Msumbiji


ZAIDI ya watu 90 waliokuwa wakikimbia ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu wamefariki dunia baada ya boti yao kupinduka kaskazini mwa Msumbiji Jana.

Mamlaka nchini humo zimesema wasafiri hao walikuwa wakitoka Lunga kuelekea Kisiwa cha Msumbiji, kando kidogo ya pwani ya Nampula.

DW imeripoti kuwa, Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya huko, mashua hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchukuwa watu 100, lakini wakati inazama ilikuwa imepakia watu wapatao 130.

Shirika la habari la AIM limeripoti kuwa chombo hicho kilipigwa na dharuba kali wakati kikiwa katikati ya mkondo.

Hivi sasa Msumbiji inakabiliwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu, ambao haujawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya robo karne, kwa mujibu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).
Ajali ya boti yauwa zaidi ya watu 90 Msumbiji Ajali ya boti yauwa zaidi ya watu 90 Msumbiji Reviewed by Zero Degree on 4/08/2024 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.