Loading...

Maji yanazidi kuongezeka wananchi chukueni tahadhari - Meja Gowelle


Watu wawili wamepoteza maisha huku kaya 628 zikiwa hazina makazi kutokana na mafuriko yanayoendelea wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kusini mwa Tanzania.

Mafuriko yalianza tangu Machi 5, mwaka huu baada ya maji kufunguliwa kutoka kwenye bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere ambalo limefurika pomoni kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kote nchini Tanzania tangu mwishoni mwa mwaka jana.

Mkuu wa wilaya ya Rufiji Meja Edward Gowelle anasema wanaendelea kuchukua tahadhari kuwanasuru wananchi waliokwama maeneo yaliyozingirwa na maji huku wale ambao tayari wameshahamishiwa maeneo salama wakiendelea kupatiwa misaada ya kibinadamu kama chakula na malazi.

Changamoto kubwa inayowakabili kwa sasa ni hatari ya magonjwa ya mlipuko kutokana na maji yaliyo zingira eneo kubwa la wilaya hiyo.

Mradi wa kufua umeme wa bwawa la Mwalimu Nyerere ulipingwa vikali na watetezi na wanaharakati wa mazingira ndani na nje ya nchi hiyo kabla ya kuanza kwake lakini serikali ya Tanzania chini ya hayati John Pombe Magufuli ulitupilia mbali mapingamizi hayo na kueleza mradi huo ni muhimu sana kwa Tanzania hasa kwa Tanzania ya viwanda aliyokua akiitaka.
Maji yanazidi kuongezeka wananchi chukueni tahadhari - Meja Gowelle Maji yanazidi kuongezeka wananchi chukueni tahadhari - Meja Gowelle Reviewed by Zero Degree on 4/08/2024 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.