Che Malone hataki kuondoka Simba - Amadou
BAADA ya tetesi kuwa beki wa kati wa Simba, Che Fondoh Malone, kuwa anataka kuondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu, wakala wa mchezaji huyo, Amadou Fontem Tigana, amesema mchezaji huyo atasalia kwenye kikosi hicho kipindi chake chote cha mkataba, labda klabu yenyewe imuuze.
Akizungumza kutoka nchini Cameroon, kutokana na madai hayo, alisema baadhi ya wanahabari walimnukuu vibaya, badala yake alisema atacheza kwa juhudi kubwa ili klabu kubwa zimnunue.
"Hajasema kuwa haipendi Simba na wala hataki kuondoka Simba, bali watu wamemtafsiri vibaya, alichosema ni kwamba atacheza kwa juhudi ili klabu kubwa zimnunue," alifafanua wakala huyo.
Ufafanuzi huo unakuja siku moja tu baada ya baadhi ya vyombo vya habari kudai kuwa beki huyo aliyejiunga na klabu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Coton Sports ya Cameroon, kuripoti kuwa ameandika barua ya kuomba kuondoka klabuni hapo mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu msimu huu.
Msimu utakapomalizika, mchezaji huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili, atabakisha msimu mmoja, hivyo klabu yoyote inayomhitaji itabidi iongee na Simba.
Huyo ni mchezaji wa pili wa Simba kuhusishwa kuondoka mwishoni mwa msimu, baada ya beki mwingine wa kati, Henock Inonga, kudaiwa kutakiwa na Klabu ya FAR Rabati ya Morocco inayonolewa na Kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi.

Reviewed by Zero Degree
on
4/10/2024 02:40:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/10/2024 02:40:00 PM
Rating: