Chimbuko la uhasama kati ya Israel na Iran
Hofu ya kupanuka kwa vita Mashariki ya Kati, kati ya Israel na Iran inazidi kukua hivi sasa.
Iran ameahidi kujibu mauji ya Jumatatu ya makamanda wake wakuu wa kijeshi - katika shambulio la Israel dhidi ya ubalozi wake mdogo mjini Damascus.
Hofu imetanda kwenye mitaa ya Israel. Baadhi ya wananchi wakikimbilia kuchukua maji na vitu vingine vya muhimu.
Kadhalika, jeshi limeitisha wanajeshi wa ziada na huduma za GPS zimezuiwa ili kutatiza ungiaji wa ndege zisizo na rubani na makombora.
Israel na Iran zimekuwa katika mizozo kwa miaka. Mivutano yao yamekuwa mojawapo ya vyanzo vya ukosefu wa utulivu katika Mashariki ya Kati.
Israel na Iran zimekuwa katika mizozo kwa miaka. Mivutano yao yamekuwa mojawapo ya vyanzo vya ukosefu wa utulivu katika Mashariki ya Kati.
Kwa Tehran, Israel haina haki ya kuwepo. Watawala wake huiona ni ‘shetani mdogo’ mshirika wa Marekani katika Mashariki ya Kati, ambayo wanaiita “Shetani mkuu,” na wanataka wote wawili watoweke katika eneo hilo.
Israel inaishutumu Iran kwa kufadhili vikundi vya kigaidi na kufanya mashambulizi dhidi ya maslahi yake.
Uhasama huo umesababisha vifo, mara nyingi ni matokeo ya operesheni za siri ambapo hakuna serikali inayokubali imehusika. Na vita vya Gaza vimefanya mambo kuharibika zaidi.
Chanzo: BBC
Chimbuko la uhasama kati ya Israel na Iran
Reviewed by Zero Degree
on
4/05/2024 02:15:00 PM
Rating: