Loading...

Kina cha Bahari ya Hindi chaongezeka



Serikali imeeleza kuwa kina cha maji ya Bahari ya Hindi kimeongezeka kutokana na kuendelea kupanda kwa joto la dunia linalosababisha kuyeyuka kwa barafu katika maeneo mbalimbali ya duniani.

Hayo yameelezwa leo Ijumaa Aprili 5, 2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo wakati akijibu swali la Mbunge wa Moshi Vijini, Profesa Patrick Ndakidemi.

Katika swali Profesa Ndekidemi amehoji iwapo kuna ukweli kwamba kina cha maji ya Bahari ya Hindi hapa Tanzania kimeongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi na nini athari zake.

Akijibu swali hilo la msingi, Dk Jafo amesema ni kweli kina cha maji ya Bahari ya Hindi hapa Tanzania kimeongezeka kutokana na kuendelea kupanda kwa joto la dunia.

Amesema kwa mujibu wa utafiti na vipimo vilivyopo, maji ya Bahari ya Hindi katika pwani ya Dar es Salaam yanaongezeka kwa wastani wa kiasi cha 6mm kwa mwaka tangu mwaka 2002.

"Athari za kuongezeka kwa kiwango cha maji ya Bahari ni pamoja na kuongezeka kwa mmomonyoko na upotevu 
wa fukwe, uharibifu wa miundombinu kama vile gati za bandari, barabara, nyumba ofisi na masoko na upotevu wa bioanuwai muhimu ikiwemo mikoko na nyasi bahari," amesema.

Ametaja athari nyingine ni upotevu wa ardhi ya kilimo na makazi, na visima vya maji baridi kuingiwa na maji ya chumvi na mafuriko ya mara kwa mara.
Kina cha Bahari ya Hindi chaongezeka Kina cha Bahari ya Hindi chaongezeka Reviewed by Zero Degree on 4/05/2024 02:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.