Loading...

City yaanza kusaka mbadala wa Pep Guardiola

Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola

Mabosi wa Manchester City wameanza kujiandaa na maisha bila ya kocha Pep Guardiola ambapo kwa kutafuta mbadala wake.

Mkataba wa sasa wa Guardiola unamalizika mwaka 2025 na awali aliripotiwa kwamba anaweza akasaini mwingine, ingawa mazungumzo bado yanaendelea.

Hadi kufikia mwisho wa msimu huu atakuwa ameifundisha timu hiyo kwa misimu tisa na anaweza akaendelea kuwepo, lakini matajiri wa timu hiyo hawaamini kwamba atakaa muda mrefu, hivyo wameanza kuchukua tahadhari.

Kocha anayeonekana kuwa katika rada za kuchukua mikoba ya Pep ni Michel Sanchez anayeifundisha Girona.

Kwa sasa Girona inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania (La Liga) na ipo katika hatua nzuri ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya licha ya kuwa imecheza ligi hiyo kwa misimu minne.

Michel amejizolea sifa lukuki kwa uwezo wa kuwaongoza wachezaji ambao walionekana kuwa wa kawaida na kumpa matokeo mazuri yaliyoiweka timu hiyo katika nafasi nne za juu.

Taarifa zinaeleza kwamba kuna urahisi wa kumpata kocha huyo kwa sababu Girona pia inamilikiwa na City Football Group ambayo ni miongoni kampuni zinazoimiliki Manchester City.

Chanzo: Mwanaspoti
City yaanza kusaka mbadala wa Pep Guardiola City yaanza kusaka mbadala wa Pep Guardiola Reviewed by Zero Degree on 4/20/2024 09:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.