Loading...

Dkt. Biteko kumwakilisha Rais Samia, mazishi ya Mkuu wa Majeshi nchini Kenya



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, amewasili jioni hii Jijini Nairobi, Kenya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogolla aliyefariki kwa ajali ya Halikopta tarehe 18 Aprili 2024, Kaben Marakwet Mashariki mwa nchi hiyo.


Katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) Jijini Nairobi Dkt. Biteko alipokelewa na Maafisa waandamizi kutoka Ubalozi wa Tanzania, wawakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kisha kusaini Kitabu cha Maombelezo.
Dkt. Biteko kumwakilisha Rais Samia, mazishi ya Mkuu wa Majeshi nchini Kenya Dkt. Biteko kumwakilisha Rais Samia, mazishi ya Mkuu wa Majeshi nchini Kenya Reviewed by Zero Degree on 4/20/2024 08:12:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.