Loading...

Faida ya ukwaju kwa afya


Ukwaju unajuulikana zaidi kwa matumizi yake katika vyakula hasa katika maeneo ya Asia, Amerika Kusini, visiwa vya Caribean na Afrika.

Vilevile ukwaju ni maarufu katika uponyaji. Hutumika kupunguza maumivu, kutuliza usumbufu wa tumbo, na kutuliza homa.

Watafiti wa zama hizi wamegundua kuwa ukwaju unaweza kutoa faida zaidi za kiafya kuliko ilivyokuwa inajulikana hapo awali.

Katika dawa za jadi, ukwaju umetumika kutibu matatizo yanayohusiana na ini. Ulaji wa ukwaju pia hutumika kutuliza kichefuchefu.

Ukwaju unatoa kinga ya mwili kwa kuzalisha virutubisho vya procyanidins, na wataalamu wanaamini vinalinda ini na kukabiliana na magonjwa ya ini.

Chanzo: BBC
Faida ya ukwaju kwa afya Faida ya ukwaju kwa afya Reviewed by Zero Degree on 4/13/2024 09:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.