Loading...

Milioni 100 kutolewa kwa kila bao, Mamelodi Vs Yanga



Yanga wamewaahidi kutoa Sh 100Mil kwa kila bao litakalofungwa dhidi ya Mamelodi. Kumbuka, Simba na Yanga mpaka sasa zina uhakika wa kulipwa Sh 2.3Bil kama zawadi kwa kucheza hatua ya robo fainali ya Caf, lakini yeyote atakayefuzu hatua ya nusu  fainali, kiwango hicho kitaongezeka mpaka kufikia Sh 3Bil.
Wakati Yanga wanacheza mechi yao ya kwanza nyumbani dhidi ya Mamelodi Sundowns vigogo wa klabu hiyo, waliwawekea mezani kiasi cha Sh 300Mil endapo wangeshinda dhidi ya matajiri hao wa madini lakini mechi hiyo ikamalizika kwa suluhu.

Ili kuhakikisha matokeo ya sare yoyote ya kufungana 
au ushindi yayanapatikana kwenye mchezo wa ugenini utakaopigwa Ijumaa saa 3:00 usiku, matokeo ambayo Yanga wanahotaji ili kufuzu hatua ya nusu fainali, Kigogo wa Yanga, GSM ameongeza dau zaidi akiwaambia mastaa wao kuwa kila bao la mchezo huo litakuwa na thamani ya Shilingi milioni 100.
Milioni 100 kutolewa kwa kila bao, Mamelodi Vs Yanga Milioni 100 kutolewa kwa kila bao, Mamelodi Vs Yanga Reviewed by Zero Degree on 4/04/2024 09:24:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.