Loading...

Mvua yazuia mechi Yanga, JKT Tanzania



MVUA kubwa inayoendelea kunyesha, Dar es Salaam, imesababisha mechi ya Ligi Kuu namba 125 kati ya JKT Tanzania iliyokuwa mwenyeji wa Mabingwa Watetezi, Yanga, iliyokuwa ichezwe jana jioni kuahirishwa kutokana na baadhi ya sehemu ya Uwanja wa Meja Jenerali, Isamuhyo uliopo Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam kujaa maji.

Akitangaza kuahirishwa mechi hiyo, Kamisaa wa mchezo huo, Kamwanga Tambwe, alisema mechi hiyo imeahirishwa baada ya kujiridhisha kuwa uwanja hauko katika hali nzuri ya kuweza kuruhusu mchezo huo kupigwa kikanuni.

Alisema kutokana na hali ya uwanja kuwa mbaya, kwa kushauriana na wenzake wameamua kuahirisha mchezo huo, na taarifa zitapelekwa Shirikisho la Sona nchini (TFF) na Bodi ya Ligi kwa maamuzi zaidi.

"Kanuni zinasema mechi ikiahirishwa kama hivi inaweza kurudiwa kesho (leo), au siku nyingine itakayopangwa, lakini kama ulikuwa umechezwa hata kwa sekunde moja, au zaidi, basi ilikuwa ni lazima mchezo urudiwe kesho, kwa maana hiyo, tunapeleka taarifa juu, huko wao ndio wataamua kwa mujibu wa kanuni zikavyowaelekea, lakini sisi tumejiridhisha kuwa mchezo hauwezi kuchezwa.

Timu zote mbili zilikuwa zimefika uwanjani zikifanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo huo, lakini kilichokuwa kinaonekana ni eneo la katikati ya uwanja ndilo lililokuwa na maji yaliyotuama, huku maeneo mengine yalionekana kuwa yako vizuri.

Mechi hiyo inaingia katika rekodi ya kuwa ya kwanza kuahirishwa kwa sababu ya sababu za akiasili msimu huu.

Awali, kuliwa na tetesi za mchezo huo kuahirishwa mapema asubuhi, lakini Bodi ya Ligi baada ya kuangalia mazingira ilijiridhisha kuwa inaweza kuchezwa, kabla ya mvua kunyesha tena mchana na kuongeza ubovu wa miundominu kwenye uwanja huo.

Kuahirishwa kwa mechi hiyo kunafanya timu zote tatu za juu, Yanga, Azam na Simba kutocheza mechi zao wiki hii.

Simba na Azam zipo Zanzibar kucheza michuano ya Kombe la Muungano, ambalo Yanga ilijitoa kwa kile ilichodai ni kubanwa kwa ratiba ya mashindano yake, mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, pamoja na Kombe la FA.
Mvua yazuia mechi Yanga, JKT Tanzania Mvua yazuia mechi Yanga, JKT Tanzania Reviewed by Zero Degree on 4/24/2024 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.