Mwamposa amuombea Makonda ofisini kwake
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda, amekutana na kuzungumza na Kiongozi Mkuu wa Kanisa la Inuka Uangaze, Nabii Boniface Mwamposa ofisini kwake Jijini Arusha.
Nabii Mwamposa aliyeambatana na viongozi wengine wa Kanisa lake, wamempongeza Makonda kuendelea kuaminika na Rais Samia Suluhu Hassan, kumtaka kuendelea kuwatumikia wananchi kwa nguvu na jitihada zake zote.
Mwamposa na watumishi wenzake walimuombea baraka Makonda wakimsihi Mwenyenzi Mungu aendelee kumpa utashi, afya njema na nguvu za kutosha katika kuwatumikia wananchi wa Jiji la Arusha.
Mwamposa amuombea Makonda ofisini kwake
Reviewed by Zero Degree
on
4/13/2024 06:57:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/13/2024 06:57:00 PM
Rating:
