Loading...

Rais Dkt. Samia amewasili KIA, tayari kwa ajili ya kuelekea Monduli kwenye Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Sokoine


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro KIA, tayari kwa ajili ya kuelekea Wilayani Monduli Mkoani Arusha kwenye Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.




Mh. Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh. Paul Christian Makonda na Mh. Nurdin Babu, Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.


Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuungana na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na viongozi wengine wa serikali kwenye kumbukizi hiyo inayofanyika nyumbani kwa Hayati Sokoine, kijijini Enguiki wilayani Monduli.
Rais Dkt. Samia amewasili KIA, tayari kwa ajili ya kuelekea Monduli kwenye Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Sokoine Rais Dkt. Samia amewasili KIA, tayari kwa ajili ya kuelekea Monduli kwenye Kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Sokoine Reviewed by Zero Degree on 4/12/2024 12:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.