Loading...

Sina nia ya kuondoka, nina deni kubwa Yanga - Aziz Ki


“Sina nia ya kuondoka hapa nimeletwa kwa sababu maalumu kama mpango huo hautokamilika nitaendelea kusalia kuitumikia timu ninayoipenda kwa moyo wangu wote, hata fedha haitaweza kujaza upendo nilionao kwa timu.” alisema Aziz Ki.

“Rais Hersi Said alinisainisha hapa kwa sababu ana malengo ya kuona timu hii inatwaa mataji ya kimataifa hili sikuwashirikisha nitakuwa hapa kwa kufanya hayo, naomba mfahamu kwa nini aliniamini na kunileta hapa yeye pamoja na kamati yake.”

“Matokeo tuliyopata juzi yaliminyima usingizi na kukosa amani kabisa kwani nilikuwa na ndoto za kuisaidia timu kuandika rekodi mpya ya kucheza nusu fainali, lakini nimekwama na nimelichukua kama funzo mimi pamoja na timu tutarudi upya na kwa nguvu msimu ujao. Nina deni kubwa.” alisema Aziz Ki.


Aziz Ki alijiunga na Yanga msimu uliopita kwa mkataba wa miaka miwili na amebakiza miezi michache tu kuukamilisha, huku akifichua ataendelea kuwepo ndani ya kikosi cha Yanga kwa vile ameshamalizana na mabosi wake, japo alikataa kuweka bayana amesaini mkataba huo na kwa muda gani.
Sina nia ya kuondoka, nina deni kubwa Yanga - Aziz Ki Sina nia ya kuondoka, nina deni kubwa Yanga - Aziz Ki Reviewed by Zero Degree on 4/08/2024 02:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.