Siri ya Simba SC kuboronga
KOCHA Msaidizi wa Simba, Selemani Matola, amesema uchovu wa kushiriki mechi za mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kusafiri na ubutu wa mastraika wake ni moja ya sababu zilizopelekea timu yao kutolewa katika mashindano ya Kombe la FA, imeelezwa.
Simba iliondolewa katika michuano ya Kombe la FA hatua ya 16 Bora baada ya kufungwa penalti 6-5 dhidi ya Mashujaa FC, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma juzi.
Wekundu wa Msimbazi ambao ni mabingwa wa Ngao ya Jamii, kwa sasa wamebakia kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara pekee.
Matola alisema timu yao haikucheza vibaya sana katika mechi hiyo, lakini hawakuwa kwenye ubora wao kutokana na uchovu wa mechi mbili ngumu za hatua ya robo fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri lakini pia wakisafiri umbali mrefu kutoka Cairo hadi Dar es Salaam na baadaye kwenda Kigoma.
Matola alisema pia mastraika wake na wachezaji wengine walishindwa kuzitendea haki nafasi nzuri walizozipata kufunga mabao.
"Nafikiri dakika 90 tulikuwa wazuri kuliko wao hasa kipindi cha pili baada ya kuwa pungufu, tumetengeneza nafasi lakini tumeshindwa kuzitumia, unajua uchovu umechangia sana sisi kupoteza mechi hii, tumekwenda katika penalti ambayo siku zote haina mwenyewe, tumetoka katika mashindano haya.
Kama nafasi tumezipata sana lakini wachezaji wetu hawakuwa makini, angalia tulipata nafasi tatu Saido na golikipa, hata wachezaji walioingia kipindi cha pili nao walikosa, tumezichezea wenyewe nafasi, mwisho wa siku tumetolewa kwa penalti," alisema Matola.
Kocha wa Mashujaa, Mohamed Abdallah 'Bares', amewapongeza wachezaji wake akisema wametekeleza kwa usahihi maagizo aliyowapa na kuibuka na ushindi katika mechi hiyo.
"Ilikuwa mechi nzuri sana kwetu, yale ambayo wachezaji wangu nimewaagiza wameyatekeleza kwa asilimia 75. Tulijua Simba wanacheza mpira wa chini, na kwa sababu wametoka katika michuano ya kimataifa watakuwa 'moto', na mchezaji wetu mmoja (Said Makapu), akatolewa kwa kadi nyekundu, tulichofanya ni mabadiliko ya wachezaji ambao tuliwatuma nini waende wakafanye ili kuziba yale mapungufu.
Tuliongeza namba ya wachezaji nyuma, na walikuwa warefu kwa kazi moja tu ya kupiga vichwa mipira yote ya krosi ambazo wachezaji wao walikuwa wanategemea, na matokeo yake tumewadhibiti," alisema kocha huyo.
Hii ni mara ya pili kwa Simba kuondolewa na Mashujaa katika mashindano ya Kombe la FA, ilikuwa ni Desemba 26, mwaka 2018 kwenye Uwanja wa Banjamin Mkapa, Wekundu wa Msimbazi ilifungwa mabao 3-2, katika mechi ya raundi ya tatu, wakati huo ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi ya Championship).
Wekundu wa Msimbazi ambao ni mabingwa wa Ngao ya Jamii, kwa sasa wamebakia kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara pekee.
Matola alisema timu yao haikucheza vibaya sana katika mechi hiyo, lakini hawakuwa kwenye ubora wao kutokana na uchovu wa mechi mbili ngumu za hatua ya robo fainali dhidi ya Al Ahly ya Misri lakini pia wakisafiri umbali mrefu kutoka Cairo hadi Dar es Salaam na baadaye kwenda Kigoma.
Matola alisema pia mastraika wake na wachezaji wengine walishindwa kuzitendea haki nafasi nzuri walizozipata kufunga mabao.
![]() |
Kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola |
Kama nafasi tumezipata sana lakini wachezaji wetu hawakuwa makini, angalia tulipata nafasi tatu Saido na golikipa, hata wachezaji walioingia kipindi cha pili nao walikosa, tumezichezea wenyewe nafasi, mwisho wa siku tumetolewa kwa penalti," alisema Matola.
Kocha wa Mashujaa, Mohamed Abdallah 'Bares', amewapongeza wachezaji wake akisema wametekeleza kwa usahihi maagizo aliyowapa na kuibuka na ushindi katika mechi hiyo.
"Ilikuwa mechi nzuri sana kwetu, yale ambayo wachezaji wangu nimewaagiza wameyatekeleza kwa asilimia 75. Tulijua Simba wanacheza mpira wa chini, na kwa sababu wametoka katika michuano ya kimataifa watakuwa 'moto', na mchezaji wetu mmoja (Said Makapu), akatolewa kwa kadi nyekundu, tulichofanya ni mabadiliko ya wachezaji ambao tuliwatuma nini waende wakafanye ili kuziba yale mapungufu.
Tuliongeza namba ya wachezaji nyuma, na walikuwa warefu kwa kazi moja tu ya kupiga vichwa mipira yote ya krosi ambazo wachezaji wao walikuwa wanategemea, na matokeo yake tumewadhibiti," alisema kocha huyo.
Hii ni mara ya pili kwa Simba kuondolewa na Mashujaa katika mashindano ya Kombe la FA, ilikuwa ni Desemba 26, mwaka 2018 kwenye Uwanja wa Banjamin Mkapa, Wekundu wa Msimbazi ilifungwa mabao 3-2, katika mechi ya raundi ya tatu, wakati huo ikiwa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza (sasa Ligi ya Championship).
Chanzo: Nipashe
Siri ya Simba SC kuboronga
Reviewed by Zero Degree
on
4/11/2024 08:10:00 AM
Rating: