Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Aprili, 2024

Crysencio Summerville, 22

Bayer Leverkusen wameungana na Liverpool na Tottenham katika harakati za kumsajili winga wa Leeds United Mholanzi, Crysencio Summerville, 22. (Bild)

Wakala wa mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres anasema itakuwa vigumu kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kusalia Sporting Lisbon ikiwa meneja Ruben Amorim, ambaye anahusishwa na Liverpool, ataondoka katika klabu hiyo. (A Bola)

Meneja wa Lille, Paulo Fonseca anaongoza orodha ya wanaozingatiwa na West Ham kuchukua nafasi ya umeneja ikiwa The Hammers wataachana na David Moyes katika majira ya joto. (I)

Klabu ya Aston Villa wanazidi kuwa na matumaini kuwa kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 25, atasaini mkataba mpya wa muda mrefu. (Talksport)

Chelsea inamlenga mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 25, msimu huu wa joto lakini klabu hiyo itahitaji kwanza kuuza wachezaji ili kupata fedha.(Football Transfers)

Meneja wa klabu ya Chelsea, Mauricio Pochettino

Mkufunzi wa Chelsea Mauricio Pochettino na makocha wake hawajafurahishwa na mchezo wa fowadi wa Ukraine Mykhaylo Mudryk mwenye umri wa miaka 23 msimu huu na The Blues watakuwa sokoni kutafuta winga mpya msimu huu. (Football Insider)

Shakhtar Donetsk wanajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Ukraine Georgiy Sudakov, huku Liverpool, Aston Villa, Arsenal na Manchester City wakimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (HITC)

Beki wa Inter Milan Denzel Dumfries anaweza kuwa analengwa na Aston Villa na klabu hiyo ya Italia itazingatia ofa ya zaidi ya euro 30m kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi, 27, ambaye mkataba wake na klabu hiyo ya Serie A unamalizika 2025. (Calciomercato)

Manchester United itawaacha wachezaji 12 wa kikosi chao cha kwanza kuondoka Old Trafford katika hatua ambayo itakuwa kubwa katika kuunda timu mpya ya klabu hiyo msimu huu wa joto. (FourFourTwo)

Kipa wa Ujerumani Alexander Nubel, 27, anatazamiwa kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na Bayern Munich ambao utahusisha kuendeleza mkataba wake wa mkopo na Stuttgart kwa msimu mwingine. (Bild)

Mshambuliaji wa Brentford na England, Ivan Toney, 28

Arsenal na Chelsea wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28, ambaye atagharimu hadi £40m msimu huu wa joto. (Florian Plettenberg)

Washirika wa 777, mwekezaji anayejaribu kuchukua udhibiti wa Everton, ameahirisha tarehe iliyolengwa ya kukamilisha mpango huo huku ikijaribu kukusanya mamia ya mamilioni ya pauni kuufadhili.(Sky News)

Makubaliano yameafikiwa kwa mkufunzi wa Lyon, Sonia Bompastor kuwa meneja ajaye wa klabu ya Chelsea ya Ligi Kuu ya Wanawake msimu huu akirithi mikoba ya meneja wa sasa wa klabu hiyo, Emma Hayes. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 11 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/11/2024 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.