Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 12 Aprili, 2024
Mshambulizi wa Sporting Lisbon na Uswidi Viktor Gyokeres analengwa zaidi na Arsenal lakini kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ina kipengele cha kutolewa cha euro 100m (£85.4m). (Football Transfers)
Brentford wanatarajia mshambuliaji wa Uingereza Ivan Toney kuondoka katika klabu hiyo msimu wa joto, lakini The Bees watadai pauni milioni 50, huku Manchester United wakiwa miongoni mwa vilabu kadhaa vya Premier League vinavyomfuatilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (HITC)
Sir Jim Ratcliffe amefanya mazungumzo ya ana kwa ana na mmiliki mwenza wa Newcastle United Amanda Staveley katika kujaribu kufikia makubaliano juu ya uhamisho wa mkurugenzi wa michezo Dan Ashworth kwenda Manchester United. (Times)
Hali nzuri ya mchezo wa fowadi wa Arsenal Kai Havertz, 24, imewafanya The Gunners kufikiria upya mipango yao ya uhamisho wa majira ya joto, huku kukiwa na uwezekano wa kilabu hiyo kuacha mipango ya kumnunua Toney. (Mirror)
Mfaransa Raphael Varane, 30, hatapewa mkataba mpya kwa pesa sawa na Manchester United na anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mkataba wake wa sasa utakapokamilika mwezi Juni.(Chris Wheeler, Mail)
Kiungo wa kati wa Arsenal Mwingereza Charlie Patino, 20, yuko tayari kwa uhamisho wa majira ya joto nje ya nchi. (Evening Standard)
Mabosi wa Newcastle wameweka pauni milioni 37 kwa klabu ikiwa ni toleo jipya la hisa, ingawa haijabainika iwapo fedha hizo zitachangia katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Mabosi wa Newcastle wameweka pauni milioni 37 kwa klabu ikiwa ni toleo jipya la hisa, ingawa haijabainika iwapo fedha hizo zitachangia katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Liverpool wamekubaliana na kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim. (Football Insider)
Meneja wa Tottenham Ange Postecoglou ameweka beki mpya wa kati kuwa mojawapo ya vipaumbele vyake vya uhamisho na mchezaji wa kimataifa wa Ecuador wa Bayer Leverkusen Piero Hincapie, 22, yuko kwenye orodha yake fupi. (Bild)
Spurs pia wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Union Saint-Gilloise na Algeria Mohamed Amoura msimu huu wa joto lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa West Ham na Wolves kwa mchezaji huyo wa miaka 23. (NipeSport)
Chelsea wanaweza kutarajia kusajili wachezaji 11 msimu huu wa joto wanapojaribu kupunguza kikosi chao kikubwa, huku kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, akiwa miongoni mwa wale wanaotarajiwa kuondoka. (Sun)
Barcelona wanajiandaa kumpa kiungo wa kati wa Uhispania Pedri, 21, ambaye amekataa ofa ya Paris St-Germain , nyongeza ya kandarasi. (Fabrizio Romano)
Manchester United na Newcastle wameripotiwa "kuanzisha mazungumzo" na kiungo wa kati wa Juventus na Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye anaweza kupatikana kwa uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Calciomercato)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 12 Aprili, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
4/12/2024 08:40:00 AM
Rating:
