Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 19 Aprili, 2024
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji Romelu Lukaku anatarajiwa kurejea Chelsea mwishoni mwa msimu wake wa mkopo wa muda mrefu nchini Italia huko Roma, ambayo haiwezi kumudu kiasi cha euro milioni 43 kumsajili mchezaji huyo wa miaka 30 kwa mkataba wa kudumu. (Gazzetta dello Sport)
Hata hivyo, klabu ya Bayern hawana nia ya kumuuza Musiala na wanatayarisha ofa ya mkataba mpya kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Fabrizio Romano)
Arsenal inamfuatilia mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko mwenye umri wa miaka 20 huku wakiongeza juhudi za kusajili mshambuliaji msimu huu. (Standard)
Klabu za Chelsea na Manchester United pia wanamfuatilia Sesko, ambaye ana kipengele cha kutolewa cha euro milioni 50. (Ben Jacobs)
Meneja msaidizi wa Liverpool Pep Lijnders ananyatiwa na klabu ya Besiktas kwa ajili ya nafasi ya kocha mkuu wa timu hiyo ya Uturuki iliyo wazi. (Athletic)
Liverpool na Paris St-Germain wanafikiria kumnunua mlinzi wa Chelsea na Uingereza Levi Colwill, 21. (GiveMeSport)
Klabu ya Tottenham wanavutiwa na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry, huku Bayern Munich wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, 28.
Spurs pia wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa Nottingham Forest Morgan Gibbs-White, 24, na wako tayari kumnunua Muingereza huyo msimu wa majira ya joto. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala anaibuka kama shabaha kuu ya Manchester City msimu wa joto, huku Chelsea pia wakifuatilia hali ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani.
Arsenal wanatazamia kumsajili mshambuliaji na winga katika msimu wa joto, huku mshambuliaji wa Newcastle Uswidi Alexander Isak, 24, na winga wa Ufaransa Michael Olise, 22, ambaye yuko Crystal Palace, wakiwa miongoni mwa malengo yao. (Guardian)
Chelsea na Newcastle United wanavutiwa na mlinda lango wa Arsenal na Uingereza Aaron Ramsdale, 25. (CaughtOffside)
Kocha wa zamani wa Liverpool na Everton Rafael Benitez anatazamiwa kuinoa Sao Paulo mwezi mmoja baada ya kutimuliwa na Celta Vigo. (Sun)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 19 Aprili, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
4/19/2024 09:26:00 AM
Rating:
