Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 14 Aprili, 2024
Inter Milan wanavutiwa na mlinzi wa Manchester United na England Aaron Wan-Bissaka, 26, ikiwa beki wa kulia wa Uholanzi Denzel Dumfries, 27, ataondoka Serie A msimu huu. (Gazzetta dello Sport)
Manchester United wanapanga kumuuza winga wa Brazil Antony, 24, msimu wa joto kwa kiwango "kinachokubalika", huku winga wa Crystal Palace Mwingereza Michael Olise, 22 akiwindwa na United. (Rudy Galetti)
Tottenham wanaripotiwa kuwa tayari kuongeza juhudi zao za kumsajili kiungo wa kati wa Atalanta Mbrazil, Ederson mwenye umri wa miaka 22.
Arsenal wana nia ya kuleta mshambuliaji ili kutoa ushindani kwa fowadi wa Brazil Gabriel Jesus, 27, na kiungo wa kati wa Ujerumani Kai Havertz, 24, huku fowadi wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, 22, akiwa miongoni mwa walengwa wao wakuu. (TeamTalk)
Kocha wa Sporting Lisbon Ruben Amorim atapewa muda wa kutekeleza mtindo wake wa uchezaji Liverpool iwapo atakuwa meneja wao mpya. (Football Insider)
Beki wa Uingereza Lewis Hall, 19, ambaye yuko kwa mkopo Newcastle United kutoka Chelsea, anatarajiwa kuondoka The Blues msimu huu wa joto kwa uhamisho wa kudumu kwenda St James' Park.
Manchester United imeibuka kuwa anayeweza kuwa mnunuzi wa mshambuliaji wa Brentford na England Ivan Toney, 28. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher, 24, anakubali kwamba atalazimika kuondoka Chelsea msimu huu wa joto ikiwa hatapewa kandarasi mpya kabla ya mwisho wa msimu huu. (HITC)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 14 Aprili, 2024
Reviewed by Zero Degree
on
4/14/2024 09:50:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/14/2024 09:50:00 AM
Rating:

.jpeg)