FIFA yaifungia Yanga SC kusajili
WAKATI ikijipanga kuhakikisha inashinda kila mechi watakayocheza, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga imefungiwa kufanya usajili wa wachezaji kwa sababu imekiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), imefahamika.
Hata hivyo FIFA na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hazikutaka kuweka wazi jina la mchezaji ambaye usajili wake umesababisha Yanga kukumbana na adhabu hiyo.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema jana uamuzi wa kuifungia Yanga umefikiwa baada ya klabu hiyo ya Mitaa ya Jangwani na Twiga, Dar es Salaam kukiuka “Annex 3 “ ya Kanuni ya Uhamisho wa mchezaji (RSTP) ya FIFA.
Ndimbo alisema pamoja na masuala mengine Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika mfumo wa usajili (TMS) licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.
"Klabu hiyo imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni na kuwasilisha taarifa kwa sekretarieti ya Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.
Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), pia imeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani,” alisema Ndimbo.
Lakini pia TFF haijafafanua adhabu ya kufungiwa Yanga itakuwa ya muda gani, kama usajili wa dirisha kubwa pekee, au mpaka pale itakapotimiza yaliyoagizwa na FIFA hata kabla ya dirisha la usajili kukamilika.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo, alisema jana uamuzi wa kuifungia Yanga umefikiwa baada ya klabu hiyo ya Mitaa ya Jangwani na Twiga, Dar es Salaam kukiuka “Annex 3 “ ya Kanuni ya Uhamisho wa mchezaji (RSTP) ya FIFA.
Ndimbo alisema pamoja na masuala mengine Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika katika mfumo wa usajili (TMS) licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.
![]() |
| Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Clifford Ndimbo |
Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), pia imeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani,” alisema Ndimbo.
Lakini pia TFF haijafafanua adhabu ya kufungiwa Yanga itakuwa ya muda gani, kama usajili wa dirisha kubwa pekee, au mpaka pale itakapotimiza yaliyoagizwa na FIFA hata kabla ya dirisha la usajili kukamilika.
Kuelekea mechi dhidi ya Singida Fountain Gate, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amewasifu wachezaji wake wanavyopambana mazoezini ili kuhakikisha wanakuwa imara na tayari kupata ushindi katika michezo yao iliyoko mbele.
Gamondi alisema hata katika michezo ambayo hawakupata ushindi, nyota wake hupambana na kinachowazuia ni suala la bahati.
“Ukiangalia wachezaji wanavyocheza unaona kabisa wanavyojitoa kwa ajili ya timu yao, tunapokosa ushindi tunakuwa tumekosa bahati tu lakini wachezaji wanakuwa wamefanya kazi yao kwa uhakika,” alisema Gamondi.
Kocha huyo alisema kila wanapokuwa kwenye uwanja wa mazoezi wanatumia muda mwingi kusisitiza kuhusu hali ya upambanaji ili kupata matokeo mazuri kwa ajili ya kutimiza malengo.
Aliongeza asilimia kubwa anaridhishwa na viwango vya nyota wake ukiacha makosa madogo madogo ambayo huwa anayaona na anayarekebisha.
“Tunatambua kila timu ipo katika mashindano hivyo imejiandaa vizuri, utakuwa mchezo mgumu lakini tunahitaji ushindi kuhakikisha tunatetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara,” Gamondi alisema.
Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inaongoza ikiwa na pointi 52 zilizovuna katika michezo 20 wakati Singida Fountain Gate iko nafasi ya saba, imejikusanyia pointi 24 baada ya kushuka dimbani mara 21.
Yanga ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya Kombe la FA.

Chanzo: Nipashe
FIFA yaifungia Yanga SC kusajili
Reviewed by Zero Degree
on
4/14/2024 10:05:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
4/14/2024 10:05:00 AM
Rating: