Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Aprili, 2024

Bernado Silva, 29

Real Madrid wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Manchester City na Ureno, Bernardo Silva mwenye umri wa miaka 29 msimu huu. (Star)

PSG wako tayari kuachana na nia yao ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 26, kutokana na masuala ya usawa wa kifedha michezoni.

Barcelona wanatarajiwa kumenyana na Real, huku rais wa klabu hiyo Joan Laporta akipatia kipaumbele usajili wa Silva. (Sport)

West Ham walikuwa na mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Cole Palmer, 21, kutoka Manchester City kabla ya Chelsea kumnunua msimu uliopita. (Sun)

Atletico Madrid inapania kumpa mkataba mpya mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 33, huku mkataba wake wa sasa ukikamilika 2026. (Rudy Galetti).

Arsenal, Juventus na Atletico Madrid wanawania kumsajili mshambuliaji wa Mexico Santiago Gimenez, 23, ambaye yuko tayari kuondoka Feyenoord ya Uholanzi. (Rekodi)

Barcelona wanatamani kumrejesha mchezaji wa zamani wa chuo chao Dani Olmo, 25, kutoka RB Leipzig. Mshambuliaji huyo wa Uhispania ana kipengele cha kutolewa cha euro milioni 60 katika mkataba wake. (Mundo Deportivo)

Klabu ya Borussia Dortmund  ya Bundesliga wako kwenye "mazungumzo" ya kuongeza mkataba wa beki wa kati wa Ujerumani Mats Hummels, ambaye atatimiza umri wa miaka 36 mwezi Desemba. (Fabrizio Romano)

Klabu ya Uturuki ya Super Lig, Galatasaray inapanga kumnunua kiungo wa klabu xa Liverpool Mholanzi Ryan Gravenberch, 21, msimu wa joto. (Fotomaki)

Joshua Zirkzee, 22

Klabu ya Manchester United na Arsenal wako tayari kuchuana na AC Milan kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee mwenye umri wa miaka 22 kutoka Bologna. (Gazetta)

Beki wa Real Madrid Nacho Fernandez ameamua kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 akitarajia kuhamia Ligi Kuu ya Soka. (Marca)

Manchester United, Juventus na Inter Milan pia ni ni baadhi ya klabu ambazo zinamvutia nahodha huyo wa Real Madrid . (Fichajes)

Kiungo wa kati wa Ureno Fabio Carvalho anatazamiwa kusalia na kupigania nafasi yake Liverpool msimu ujao chini ya kocha mpya wa klabu hiyo, licha ya kutakiwa na Hull City ambako mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anacheza kwa mkopo. (Football Insider)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 21 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/21/2024 11:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.