Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 28 Aprili, 2024

Kyle Walker, 33

Bayern Munich wanapanga uhamisho mwingine wa kumnunua mlinzi wa Manchester City Muingereza Kyle Walker, baada ya kushindwa kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 msimu uliopita wa joto. (Star)

Mmiliki mwenza wa klabu ya Manchester United Sir Jim Ratcliffe amekutana na wakala bora Jorge Mendes, ambaye wateja wake ni pamoja na mmoja wa wachezaji wanaolengwa wa klabu hiyo katika kiungo wa kati wa Benfica na Ureno Joao Neves, 19. (Mirror)

Crystal Palace wako tayari kujiunga na mbio za kumsajili beki wa kati wa Wolfsburg Mfaransa Maxence Lacroix mwenye umri wa miaka 24 msimu huu wa joto. (Telegraph)

Arne Slot atateuliwa kuwa kocha mkuu wa Liverpool badala ya kuwa meneja katika mabadiliko ya muundo wa klabu. (Times)

Matumaini ya West Ham ya kumteua kocha wa zamani wa Wolves Julen Lopetegui kuchukua nafasi ya David Moyes kama meneja msimu huu yanaonekana kukamilika huku AC Milan wakikaribia kuafikiana. (Guardian)

Barcelona wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Argentina Guido Rodriguez, 30, kutoka klabu nyingine ya La Liga ya Real Betis. (Sport)


Barcelona wanapanga kulinda mustakabali wa mlinzi wa kati Pau Cubarsi mwenye umri wa miaka 17 baada ya kupendekeza mkataba mpya kwa Mhispania huyo ambao unajumuisha kipengele cha kutolewa cha euro 500m (pauni milioni 423.2). (AS)

Kiungo wa zamani wa Manchester United na Uhispania Juan Mata, 35, anaamini kuwa klabu yake ya zamani inapaswa kujenga timu yoyote ya baadaye karibu na Bruno Fernandes wa Ureno, 29. (ESPN)

Kipa wa Ujerumani Loris Karius, 30, ataondoka Newcastle United kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu. (Fabrizio Romano)

Juventus wanashughulikia mikataba ya kuongeza kandarasi za mshambuliaji wa Italia Federico Chiesa, 26, na mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 24.

Juventus wanashughulikia mikataba ya kuongeza kandarasi za mshambuliaji wa Italia Federico Chiesa, 26, na mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic, 24. (Rudy Galetti).
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 28 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 28 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/28/2024 08:56:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.