Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Aprili, 2024


Arsenal na Manchester City wanafikiria kumnunua kiungo wa kati wa Newcastle United na Brazil Bruno Guimaraes, 26. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Ureno Bernardo Silva ameamua kuondoka klabu ya Manchester City na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ambaye ana kipengee cha kumuachilia cha pauni milioni 50 ana nia ya kuhamia klabu ya Barcelona. (Sport)

Chelsea imetaka habari kuhusu mlinzi wa kati wa RB Leipzig na Ufaransa Castello Lukeba, 21, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 60 katika mkataba wake na klabu hiyo ya Bundesliga. (FootMercato)

Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anataka klabu hiyo kumleta mshambuliaji mwingine katika majira ya joto ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Mshambulizi wa zamani wa klabu ya Arsenal na Manchester United, raia wa Uholanzi Robin van Persie anakaribia kuchukua wadhifa wake wa kwanza wa ukocha, baada ya kufanya mazungumzo na klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uholanzi Heerenveen. (Algemeen Dagblad)

Real Madrid wanapanga kumuongezea mkataba mlinzi wa Uhispania Lucas Vazquez, 32, ambaye mkataba wake wa sasa unakamilika mwezi Juni. (AS)

Klabu ya Paris St-Germain wamsaka kinda wa Barcelona mwenye umri wa miaka 16 Lamine Yamal. (Le Parisien)


Beki wa Chelsea Thiago Silva, 39, amefikia makubaliano ya mdomo na Fluminense , huku Mbrazil huyo akimaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu (Goal)

Manchester United wanavutiwa na mlinzi wa Inter Milan na Italia Alessandro Bastoni, 25, na wako tayari kutoa takriban £52m. (Fichajes)

Klabu ya Uholanzi Feyenoord inavutiwa na winga wa Tottenham mwenye umri wa miaka 23 Bryan Gil, ambaye anatarajiwa kuondoka Spurs msimu wa joto. (Standard)

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Olivier Giroud, 37, atatia saini mkataba na klabu ya Ligi Kuu ya Soka (MLS) Los Angeles FC na atajiunga nao kwa uhamisho wa bure msimu wa joto wakati mkataba wake wa AC Milan utakapokamilika. (RMC Sport)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/24/2024 01:51:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.