Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 4 Aprili, 2024

Beki wa klabu ya Bayer Leverkusen, Jeremie Frimpong

Arsenal, Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa klabu za Ligi Kuu ya England zinazomuwania beki wa Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong. Mholanzi huyo, 23, atapatikana kwa pauni milioni 35 msimu wa majira ya joto.

Tottenham pia wameungana na Arsenal katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 24, iwapo Newcastle italazimika kuuza wachezaji wake muhimu msimu huu wa majira ya joto. 

Tottenham pia wameungana na Arsenal katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uswidi, Alexander Isak

Newcastle itapatia kipaumbele usajili wa mabeki wawili wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa baada ya Mholanzi Sven Botman, 24, na Muingereza Jamaal Lascelles, 30, kukabiliwa na majeraha ya muda mrefu.

West Ham haina mpango wa kubadilisha mkataba wa mkopo wa Phillips kuwa wa kudumu katika klabu hiyo. (Football Insider)

Newcastle United wanahofia huenda wakahitaji kumuuza kiungo wa Brazil Bruno Guimaraes, 26, ili kukidhi sheria za kifedha za Ligi kuu ya Uingereza. Miamba ya Ufaransa Paris St-Germain wanaongoza katika mbio hizo, huku Manchester United na Arsenal pia wakiwa na hamu ya kupata saini ya nyota huyo. (Sun)

Mshambuliaji wa Uswidi Viktor Gyokeres, 25, yuko juu kwenye orodha ya washambuliaji wa Arsenal, lakini Sporting Lisbon wanatarajia kipengele cha kuachiliwa kwa mchezaji huyo cha euro 100m (pauni 85.6m) kuchochewa ili aondoke. (Caught Offside)

Kalvin Phillips, 28

Kiungo wa kati wa Uingereza Kalvin Phillips, 28, atalazimika kukatwa mshahara mkubwa ikiwa anataka kondoka katika klabu ya Manchester City na kurejea Leeds United msimu huu wa majira ya joto. (Mirror)

Kalvin Phillips bado hajafunga bao katika mechi tisa alizoichezea West Ham

Manchester United wameanza majadiliano kuhusu kumsajili beki wa Nice mwenye umri wa miaka 23 Melvin Bard, huku wakilenga kusajili beki mpya. (Evening Standard)

Beki wa Wolves Muingereza Max Kilman, 26, pia yuko kwenye orodha ya wachezaji wanaowania uhamisho wa majira ya kiangazi ya Manchester United. (Times)

Leicester City wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Arsenal na raia wa Uingereza, Eddie Nketiah mwenye umri wa miaka 24, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Crystal Palace na Brentford. (Football Transfers)

Klabu ya Newcastle wanavutiwa na kiungo wa kati wa Real Madrid Muhispania Dani Ceballos, 27. (Mundo Deportivo)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 4 Aprili, 2024 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 4 Aprili, 2024 Reviewed by Zero Degree on 4/04/2024 08:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.