Nusu fainali CAF: TP Mazembe, Al Ahly hakuna mbabe
Sare isiyo ya mabao waliyoipata watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri wakiwa ugenini dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo, imeiweka pazuri timu hiyo ya Misri katika na nafsi ya kutinga fainali ya 17 tangu mwaka 1987.
Katika mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali iliyopigwa jioni ya leo Jumamosi kwenye Uwanja wa TP Mazembe uliopo jijini Lubumbashi, Ahly iliwabana wenyeji wao walitwaa taji hilo mara tano ikiwa ni moja ya klabu mbili zinazoshika nafasi ya pili nyuma ya Wamisri hao waliotwaa mara 11.
Al Ahly imeshacheza fainali 16 hadi sasa, zikiwamo tano ilizopoteza na 11 ilizotwaa taji ikiwamo ya msimu uliopita na sasa inahitaji ushindi ikiwa nyumbani ili kutinga fainali ya 17 na kusibiri kujua itcheza na nani kati ya Esperance ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zitakazovaana usiku huu katika pambano jingine la nusu fainali jijini Tunis, Tunisia.
Pambano la Lubumbashi limekuwa ni la tano kwa Mazembe na Al Ahly kukutana katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika tangu mwaka 2000, huku rekodi zikiwabeba Wamisri wakicheza nyumbani kwani mechi zote mbili zilizopita kati ya nne za awali walizokutana imeshinda. Al Ahly ilishinda nyumbani mechi ya kwanza kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa Sept 01, 2002 kisha kurudia tena July 08, 2012 kwa mabao 2-1.
Katika mchezo huo wa Lubumbashi, timu zote zitajilaumu kwa kushinda kutoka na mabao kwani, kila moja zilitengeneza nafasi nyingi zilizoshindwa kukwamisha wavuni, lakini imekuwa faida zaidi kwa Al Ahly ambao walionekana kushangilia sana mara baada ya filimbi ya mwamuzi Pacifique Ndabihawenimana kutoka Burundi.

Mechi zilizopita Mazembe vs Al Ahly
- Apr 20, 2024 Mazembe 0-0 Al Ahly
- Sept 02, 2012 Mazembe 2-0 Al hly
- July 08, 2012 Al Ahly 2-1 Mazembe
- Sept 14, 2002 Mazembe 0-0 Al Ahly
- Sept 01, 2002 Al Ahly 1-0 Mazembe.
Nusu fainali CAF: TP Mazembe, Al Ahly hakuna mbabe
Reviewed by Zero Degree
on
4/21/2024 08:12:00 AM
Rating: