Wanasimba tuwe wavumilivu - Ahmed
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa wavumilivu katika kipindi ambacho timu hiyo inapitia wakati mgumu.
Ahmed Ally ameyasema hayo kupitia mtandao wa Instagram ambapo ameeleza kuwa "Dhahabu hupitishwa kwenye moto mkali ili ipate thamani na iwe bora, licha ya kuwa huteseka inapopita kwenye moto huo lakini mwishoe hubaki safi, bora na thamani yake huongezeka maradufu".
"Wana Simba tuvumilie kupita kwenye moto huu mkali ili tuwe bora na hadhi yetu irejee, najua maumivu ni makubwa kwa kuwa moto mkali lakini hatuna budi kuvumilia kwani ndio njia pekee ya kurudi kwenye thamani yetu," Ameeleza Ahmed
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wanasimba tuwe wavumilivu - Ahmed
Reviewed by Zero Degree
on
4/22/2024 10:12:00 AM
Rating:
